Leo ukiangalia ndoa nyingi zimepooza na kufunikwa na wingu zito la mizozo kila kukicha,ukiwauliza wanandoa wengi husema Mwanzoni mwa ndoa yetu tulipendana kwa dhati,lakini shauku na penzi letu siku hizi imepotea,hakuna urafiki mzuri kati yetu kama hapo awali wala hatufurahii kuwa pamoja,hata kucheka inakuwa tatizo pamoja na kulala kitanda kimoja na ushirika wao katika mambo mengi, lakini mambo yanakuwa hayaendi,ndoa zingine wana ndoa hawawezi hata kujadili matatizo yao kwa pamoja,,mbaya zaidi kufanya mapenzi kwao imekuwa kama wajibu badala ya starehe,hii ni hatari maana hakuna mtu kati yao anayejisikia shauku ya mapenzi kwa mwenzi wake,ukichunguza sio kwamba kuna mtu anatoka nje ya ndoa hapana utawasikia wanasema ndoa yetu haina upendo.Matatizo ya ndoa yapo mengi na yanatofautiana ndoa na ndoa,lakini vilio vingi vya ndoa vinafanana,swali kubwa hapa ni kutaka kujua ni jinsi gani unaweza kuifurahia ndoa yako pamoja na changamoto nyingi unazokutananazo kila kukicha.Hebu tuangalie baadhi ya mambo yanayoweza kuifikisha ndoa yako kwenye furaha isiyo kifani na ya kusisimua.
Jambo la kwanza
1: UPENDO

Tatizo la watu wengi ni kwamba hawajui nini maana ya upendo, na wengi wanafikiri wanafahamu lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa kile wanacho kijua na kukiamini kuhusu upendo hakina ukweli wowote. Leo ukizunguka kila mahali utakutana na watu wengi wamechanganyikiwa kwa kutojua maana ya upendo. hili si tatizo la mtu mmoja au wawili bali ni tatizo ambalo limetapakaa dunia nzima. Ajabu ni kwamba unaweza kukuta watu wanazungumza juu ya upendo lakini kwa makini ukichunguza utaona hawajui maana yake. Leo matatizo mengi katika ndoa yanasababishwa na kutopendana kati ya mume na mke hii ni pamoja na kutojua nini maana ya upendo au penzi.

Tatizo la watu wengi ni kwamba hawajui nini maana ya upendo, na wengi wanafikiri wanafahamu lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa kile wanacho kijua na kukiamini kuhusu upendo hakina ukweli wowote. Leo ukizunguka kila mahali utakutana na watu wengi wamechanganyikiwa kwa kutojua maana ya upendo. hili si tatizo la mtu mmoja au wawili bali ni tatizo ambalo limetapakaa dunia nzima. Ajabu ni kwamba unaweza kukuta watu wanazungumza juu ya upendo lakini kwa makini ukichunguza utaona hawajui maana yake. Leo matatizo mengi katika ndoa yanasababishwa na kutopendana kati ya mume na mke hii ni pamoja na kutojua nini maana ya upendo au penzi.
Upendo ni nini? Upendo ni vitendo vya ukarimu, ni tendo tufanyalo, sio kujisikia, ni kufanya vitendo vya ukarimu na kuzungumza maneno ya upole na fadhili, upendo ni kutoa na kusameheana, ni kusaidiana, ni shukurani, ni tabasamu, ni kupongeza na vitendo vingine vingi vinavyofanana na hivi. Hapa ndio linakuja tatizo la watu wengi ambao huamini kuwa upendo ni kitu ambacho kinaweza kupotea au kutoweka. Unajua ni rahisi kusimama na kusema kuwa “Upendo au penzi letu kwenye ndoa yetu limepotea” Hapa ukweli halisi ni kwamba upendo hauwezi kupotea kwa sababu upendo au penzi ni vitendo, hivyo unaweza kuchangua kutenda vitendo vya upendo au usichague kufanya hivyo. kama utachagua kuwa mwenye huruma, kusaidia, kusema kweli hapoutakuwa umechagua kupenda, lakini bado unaweza ukachagua kutokupenda pia. Unaweza kuchagua kutokuwa na subira wala msamaha na ukachagua kutompenda mwenzi wako, hapo hauwezi kusema kuwa pendo au penzi lako limepotea. Hivyo ni vizuri mtu akatambua kuwa upendo ni kuchagua kufanya vitendo vya ukarimu.
Jambo la pili
Hisia ya penzi ni nini? Hisia ya penzi ni ile hali isiyo kifani, msisimko moyoni, na kujisikia mchangamfu na mwenye raha umwonapo mpenzi wako. Ni hisia nzuri kwa kweli kuwanayo, ni nzuri kupindukia ndiyo maana hata nyimbo na mashairi yameandikwa juu yake. Wengi wetu tumekwisha patwa na hisia hizi, Pengine ulikuwa kijana mdogo sana wakati unapatwa na hisia za mapenzi kwa mara ya kwanza. Mapigo yako yalikwenda mbio mara mia zaidi kila mara anapokutazama, na baadaye mlipoahidi kuoana na huyo ambaye hivi sasa ni mkeo au mumeo, pengine hisia zako kwa wakati huo zilikuwa na nguvu sana. Hata hivyo kuna ukweli mmoja kuhusu hisia za mapenzi ambao ni watu wachache tu wanao ufahamu, kwamba hisia za mapenzi huja na kutoweka, leo mtu anaweza kuwa na hisia za mapenzi lakini kesho zikatoweka, na baadaye kidogo zikarejea tena na pengine baada ya mda kidogo zikatoweka tena, na baadaye zikajitokeza tena, kwa nini? Kwa sababu hisia za mapenzi ni hisia tu na hisia zetu daima hubadilika. Sisi binadamu tuna hisia za aina nyingi, mara nyingine hujisikia mwenye huzuni na majonzi, lakini siku nyingine hujisikia mwenye furaha, wakati mwingine hujisikia umejawa na msisimko wa furaha, wakati mwingine hujisikia mwenye hasira na wakati mwingine hujisikia mpweke, vile vile wakati huja tunajikuta tunajisikia kupenda, lakini hatukai na hisia hiyo hiyo kila siku, hii ni kwa sababu hisia zetu zinabadilika, sijui kama kuna mtu ambaye ameshawahi kuwa mwenye furaha kila siku mwaka mzima, hili haliwezekani maana furaha ni hisia tu hivyo huja na kutoweka, ni muhimu sana kila mtu kutambua kuwa hisia zetu huja na kisha zinatoweka, na hii ni pamoja na hisia za mapenzi. Katika ndoa za kikristo bwana bibi arusi huahidi kupendana hadi watakapokufa, swali hapa, ni je kusema hivyo wanamaanisha kuwa wameahidi kuwa na hisia za mapenzi kila siku hadi kufa? Hapana, wanapo ahidi kupenda, wanakuwa wameahidi kufanyiana vitendo vya upendo kati yao kwa kipindi chote cha uhai wao, wana ahidi kuendelea kuwa wakarimu, kusaidiana, kuelewana, kusikilizana vile vile kusameheana na matendo mengine mengi ya kufanana na haya. Je, unaweza kuwa na hisia za penzi? Ndiyo, lakini sio kwa wakati wote, siku nyingine unaweza ukawa na msisimko mkali na hisia motomoto za mapenzi, lakini wakati mwingine unaweza ukawa na hisia tofauti, unaweza kujisikia mwenye hofu moyoni au pengine kuvujika moyo au kukasirika na hivyo kutokuwa kabisa na hisia za mapenzi moyoni mwako, hali ya namna hii inapokutokea usiogope maana ni hali ya kawaida kabisa kutokea. Mungu hajatuamuru tuwe na hisia Fulani tu, bali ametuamuru kupenda. Kwa hiyo mume na mke lazima wa waendelee kupendana kwa vitendo, hisia zitakuja na kutoweka wala hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya hilo maana ni jambo la kitambo kidogo tu, jukumu kubwa katika ndoa ni kupendana tu kwa maneno ya upole na kwa vitendo na kuendelea kufanya hivyo kila siku. Lazima ujue hili kuwa hatuwezi kudhibiti hisia zetu bali tunaweza kudhibiti vitendo vyetu, hatuwezi kuchagua kuwa na hisia za fulani lakini tunaweza kuchagua kufanya vitendo vya aina fulani. Kwa mfano unaweza kushawishika kumkaripia mwenzi wako, lakini badala yake ukachagua kuongea naye kwa maneno ya upole, hapo utakuwa umechagua kumpenda mwenzi wako, hata kama unajisikia kuwa mchoyo na kutaka kujipendelea, unaweza bado ukachagua kumjali mwenzi wako, unaweza kumsikiliza na kujaribu kumwelewa kila anapozungumzia matatizo yake,, unaweza kuchangua kumfariji na kumtendea matendo ya upendo hata kama hisia zako zinakushawishi uwe mchoyo na mbinafsi. Kuna wakati unaweza ukajisikia kumhudumia mwenzi wako lakini pia kuna wakati unajisilia kujifurahisha mwenyewe, katika hali kama hii unachopaswa kujua ni kuwa upendo ni kumhudumia na kumjali mwenzi wako hata kama haujisikii kufanya hivyo. Unapochagua kumhudumia mwenzi wako unaweza ukawa haufuati hisia za wakati huo lakini ukawa unatimiza ahadi uliyo ahidi siku ya arusi yenu, tunaahidi kuwapenda wenzi wetu kwa sababu tunaweza kuchagua vitendo vyetu na sababu nyingine ni kwamba upendo hauko nje ya udhibiti wetu, tunaweza kupenda tukitaka.
Ufanye nini hisia za mapenzi zinapotoweka kabisa?
Hata kwenye ndoa imara hisia za mapenzi huja na kutoweka, hisia za mapenzi zinapotoweka mtajikuta hamjisikii kupendana kabisa na hali yenu kwenye ndoa yenu inakuwa mbaya sana, hili ni tatizo kubwa kabisa maana linaiweka ndoa kwenye hatari na muyumbo mkubwa sana. Ndoa yako ikifikia hatua kama hii basi kumbuka mambo yafuatayo.
Hata kwenye ndoa imara hisia za mapenzi huja na kutoweka, hisia za mapenzi zinapotoweka mtajikuta hamjisikii kupendana kabisa na hali yenu kwenye ndoa yenu inakuwa mbaya sana, hili ni tatizo kubwa kabisa maana linaiweka ndoa kwenye hatari na muyumbo mkubwa sana. Ndoa yako ikifikia hatua kama hii basi kumbuka mambo yafuatayo.
Ø Hata kama hisia zako zimetoweka: mpende mwenzi wako wa ndoa, mpende kwa vitendo vya ukarimu na uwe mwangalifu kumsaidia, uwe mpole, mkarimu, mwaminifu na mwenye kujitoa.
Ø Kadri unavyoendelea na vitendo vya upendo ghafula utaanza kuona hisia zako za mapenzi zinarejea, huu ni ukweli kwamba hakuna haja ya kuishi pamoja katika ndoa bila hisia za mapenzi kati yenu. Hisia zenu zama penzi zitarudi iwapo tu mtaendelea kutendeana vitendo vya upendo. Hakika hisia za ampenzi ni hisia tu, hauwezi kuwanazo kila siku, zitakuja na kutoweka lakini haupaswi kuwa na wasiwasi. Kama utachagua kupenda kwa vitendo ni dhahili kuwa hisia zako za penzi haziwezi kupotea kwa mda mrefu.
Mkiacha kufanyiana vitendo vya upendo matokeo yake ni kutoweka kabisa kwa hisia zenu za mapenzi. Wanandoa wengi mda mfupi baada ya ndoa yao wanakuwa wapole na wakarimu kati yao lakini baada ya mda mfupi wanashindwa kuwa makini na wanaacha kutendeana vitendo vya upendo, badala yake wanaanza kukosoana, kukashifia, na kutoaminiana, vitendo kama hivi kwa hakika huondosha hisia za mapenzi mioyoni mwa wanandoa. Lakini mkiamua kutendeana vitendo vya upendo,msisimko wa hisia za mapenzi utarudi. Hebu tuseme wewe leo una hisia nzuri ajabu kwa mke wako mpenzi, kwa hakika ni mwanamke mzuri na wakupendeza ajabu. Lakini huyo mkeo amefanya jambo Fulani linalokuudhi sana, kadri unavyofikiria jinsi mkeo alivyokuudhi ndivyo na hisia zako za mapenzi moyoni mwako zinabadilika taratibu na kuwa hisia za hasira na chuki. Ndipo unakuja uchaguzi, kama unataka unaweza kuchagua kutokuwa na subira au msamaha kwa mkeo kwa maneno mengine ni kwamba unaweza kuchagua kutompenda mkeo, au kama ukitaka unaweza kuchagua kumfahamisha kwa njia ya upole na kumweleza jinsi alivyokuudhi na baada ya hapo ukamsamehe na kusahau, ni chaguo lako unaweza kupenda kama unataka .
Betty alifurahia sana kuolewa na George, kila siku alimshukuru sana Mungu kwa kumpa mume mkristo na mwenye haiba na tabia nzuri, ni furaha iliyoje atakayo kuwa nayo katika maisha yake yote! Baada ya miezi michache, siku moja Betty alijikuta akimwuliza Mungu, “kwa nini ulinipatia mume na kwa nini awe huyu?” Betty alikuwa amegundua kuwa George alikuwa hapendeki mda wote kama ambavyo angetaka. Hivyo hisia za Betty zikaanza kufifia moyoni, lakini baadaye Betty alikumbuka maneno ya mchungaji siku ile ya arusi, “Unaahidi kumpenda mwanaume huyu?” Ndipo akajibu, “Ni lazima nimpende George! Ni lazima ni mpende hata nyakati anaporinga na kutoafikiana nami na kuonyesha ubinafsi, nategemea naye atafanya hivyo hivyo na kuendelea kunipenda hata kama nitaonyesha jeuli na ukaidi mara nyingine.” Halafu alijiambia, “kuanzia sasa nitampenda mume wangu na nitampikia chakula akipendacho!” Na alipokuwa anapika hisia zake za mapenzi zilianza kubadilika na alinza kujisikia kumpenda kwa mara nyingine. Ni kitendo cha upendo kwa mwanamke kumpikia mume chakula akipendacho, maana vitendo vya upendo hurejesha hisia za mapenzi. Bahati mbaya wanawake na wanaume wengi hawafahamu ukweli huu, wengi huamini kuwa hisia za penzi zinapotoweka basi penzi nalo linapotea kabisa.
Ø Penzi ni kitendo, ni kitendo cha kumjali na kumfikiria mwenzi wako na kuwa mpole, muungwana, mwenye subira, na mengine mengi yanayofanana na hayo. Unaweza kupenda kama utachagua kupenda.
Ø Hisia ni hisia tu, kwa hiyo huja na kutoweka.
Ø Kama utachagua kutopenda kwa vitendo basi hisia za mapenzi zitapotea kabisa.
Ø Kama hisia zako za mapenzi zitatoweka, zirudishe tena kwa kuchagua kupenda kwa vitendo.
Jambo la tatu
Editha alimwambia kaka yake, “Nataka kumpa mume wangu talaka, nataka apate uchungu sana! Kaka yake alimwambia, “Hilo ni jambo zuri.” Nitakueleza namna ya kumwuumiza kikamilifu. Hatua ya kwanza anza kufanya juu chini, kila njia kumfurahisha, mfanyie vitendo vya ukarimu, zungumza naye kwa heshima na upendo na acha kulalamika, mara atang’amua kuwa anakutegemea na hawezi kuishi bila wewe. Halafu hatua ya pili, mpe talaka! Hakika kitendo hicho kitamuuma sana!” Baada ya miezi michache alimtaarifu kaka yake kuwa ametekeleza hatua ya kwanza. “Vyema kaka yake alijibu, sasa ni wakati wa kumpa talaka” “Talaka!” sauti ya Editha ilijawa na mshangao. “Kamwe siwezi!” Nampenda sana siku hizi, penzi letu limekuwa bichi tena!” Editha aligundua kuwa vitendo vya upendo hurudisha hisia za mapenzi. Bahati mbaya ni kwamba baadhi ya wengi waliooana hawajui wala hawajagundua ukweli huu. Wengi hufikiria kuwa wamepoteza penzi lao na hakuna chochote wawezacho kufanya kurudisha penzi lao, baada ya hapo hatua wanayo fikiria ni kupeana talaka tu, hatua ambayo pia haiwezi kukupunguzia matatizo au changamoto katika ndoa yako. Agizo la Mungu kwa wana ndoa ni kupendana na si kupeana talaka.
(1wakoritho 13:8, Yohana 15:17, Waefeso 5:25, Mathayo 19:9)
Kitu ambacho unatakiwa kukikumbuka ni ile ahadi uliyo iweka siku ya arusi yaani kupendana mpaka mauti itakapo watenganisha. Huu ndio wajibu unaotakiwa kuutekeleza, kumpenda mwenzi wako kama ulivyo ahidi. Kupenda sio rahisi, lakini kwa kuwa uliapa kumpenda mwenzi wako kwa msaada wa Mungu lazima utekeleze. Mara uanzapo kupenda kwa vitendo, utashangazwa na kujawa na furaha kuona kuwa hisia zako zimerejea, utakuwa tena na hisia za kusisimua na kushangaza, hisia zinazo weza kukufanya uimbe na kupiga kelele za furaha na kusema, “Nampenda kwa moyo wangu wote.” Baada ya hapo ni wazi kuwa hisia zako za mapenzi zitapanda na kuteremka. Wajibu wako ni kumpenda mwenzi wako kila siku bila kujali kuwa hisia zako ziko juu au chini siku hiyo. Kama utafanya kazi nzuri ya kupenda kwa vitendo hisia za upendo katika ndoa yako zitazidi kukua na kuendelea kuwa za kusisimua kadri miaka inavyopita. Daima kutakuwa na matatizo ya hapa na pale, lakini vipindi vya matatizo vitakuwa vichache zaidi ukilinganisha na vipindi vya furaha. Si rahisi kwetu kupenda maana tuna asili ya ubinafsi, ukweli ni kuwa mara nyingi huwatunajisikia kufanya au kusema vitu visivyo vya upendo. Mungu anajua jinsi ambavyo ni vigumu kupenda lakini ametuamuru kupenda na hutupa nguvu tunayohitaji kuweza kupenda. Inahuzunisha kuona kuwa mamilioni ya watu duniani wanakataa kuwa hawahitaji msaada wa Mungu, huzania kuwa wanaweza kumdu maisha yao bila msaada wake, ni wazi kabisa kuwa hawezi kuwasaidia wale wanaofikiri kuwa hawahitaji msaada wake. Kitu kingine ambacho wana ndoa wengi wamesahau ni kuwa wanapaswa kumwamini Mungu ili awasamehe dhambi zao na kupewa uwezo wa kutii amri amri za Mungu hii ni pamoja na kupenda. Kupenda si rahisi lakini kama tutaanza kwa kumpenda Mungu kwanza tunaweza kuanza kushinda vita hiyo, kwa sababu nguvu ya roho mtakatifu imo ndani yetu. Watu wengi husema, “kama utachagua kwa uangalifu mwenzi wako wa ndoa, basi kupenda kutakuwa ni kazi rahisi,” lakini ukweli ni kwamba si kazi rahisi kupenda kila siku, mwaka hadi mwaka, upendo unahitaji juhudi, lazima tuweke jitihada katika kupenda kwani kupenda ni kazi. Kwa mfano: Mvulana anapovutiwa na msichana Fulani huwa mwangalifu sana, mpole na mkarimu kwake. Na iwapo huyu msichana anvutiwa na mvulana huyo na anataka naye apendeke, hufanya jitihada awe wa kuvutia, mcheshi na mara nyingi hujaribu kuepukana na haisira na kuwa mvumilivu na mwenye kujaa subira, vitendo hivi vya upendo huendelea kwa miezi kadhaa, baada ya hapo huoana………nini hutokea baada ya kuoana? Mke hufikiria moyoni, “sasa nina mume; sina wasiwasi wa kuishi maisha yangu yote bila kuwa na mume, naweza kupumzika sasa.” Kulegea au kupumzika maana yake nini? Ina maana kuwa hajali tena kama anampendeza au hampendezi mumewe. Mume naye hufanya hivyo hivyo, badala ya kuwa mwangalifu na mwenye juhudi kufikiria mahitaji ya mwenzi wake, huanza kuzembea. Kinachotokea baada ya hapo, mmoja wapo anapoumizwa rohoni kwa maneno au kitendo Fulani, hatajaribu kusamehe wala hawi mwangalifu na husema maneno ya ukali ya kumuumiza mwenzi wake bila kujali madhara yatakayo tokea badaye. Kukumbuka kuwa ndoa yenu inaweza kuwa nzuri tu pale mmoja wenu atakapochagua kuwa mnyenyekevu na mkarimu hata hata kama hatendewi ukarimu na mwenzi wake, hii si kazi rahisi ndio maana wengi hawaifanyi, wako mapumzikoni, mara hisia za mapenzi huanza kupungua, lakini kabla ya kuoana kila mtu alikuwa mwangalifu kwa kumtendea mwenzi wake kwa ukarimu na hisia zao za mapenzi zilikuwa za kusisimua. Ili uhusiano wenu uendeelea kuwa mzuri na nyakati zenu za kwenda kitandani zijae mapenzi ya kusisimua lazima mchagua kufanyiana wema kila siku, yaaani kufanyiana vitendo vya ukarimu.
Jambo la nne
Tumeona mambo mengi juu ya upendo na hisia za mapenzi, na jambo kubwa kati ya haya yote ni kumpenda mwenzi wako hata kama haujisikii kufanya hivyo, lakini swali hapa ni kwa njia ngani utaonyesha huo upendo wako kwa mwenzi wako kila siku?
Njia ya kwanza
(a)Kuongea maneno ya shukrani
Kila mtu aliyeumbwa na Mungu anahitaji kuthaminiwa, sote tunapenda kusikia maneno haya, “Nakupenda, nafurahi kuona unajitoa kunihudumia, nashukru kuona unawapenda wazazi wangu, una roho mzuri, na furahi kwa kuwa unanipenda, nina furaha kuolewa na wewe, kila mtu anahitaji kuishi na mtu mwenye utajiri wa maneno kama haya.
Kama watu hawatupi shukrani basi tunajisikia vibaya na kuumia rohoni, Neema alisema, “Mume wangu haonyeshi kujali kama nyumba ni safi, na mashati yake yamenyooshwa, yeye anachojua ni kuuliza kama chakula kikotayari,” Tunawajibika kujali na kuonyesha shukrani kwa wenzi wetu katika kila kitu wanachokifanya, siyo tu katika faragha bali hata hadharani. Ni furaha iliyoje kupokea shukrani mbele ya marafiki! Wambura na Roda waliwatembelea ndugu zake na mume, Roda limwomba mumewe, “Tafadhali naomba unipeleke dukani mara moja kwa gari, nataka kununua nepi zaidi kwa ajili ya mototo kwani zilizopo hazitoshi.” “kwa nini hauwezi kupangilia mambo yako vizuri!” Wambura alijibu kwa ukali, “ni lini utajifunza kupangilia na kuandaa mambo yako kabla ya wakati?” Wambura aliyasema haya maneno mbele ya ndugu zake….ambao Roda alikuwa amepania kuwaonyesha jinsi ngani alivyo mke mzuri. Fikiria jinsi gani Roda angefurahia kama mumewe angetafuta neno lolote zuri la kumsifia mkewe mbele ya ndugu zake! Wambura alipoteza nafasi nzuri ya kumpenda mkewe kwa maneno ya shukrani. Je, si udanganyifu kujaribu kumsifia au kumshukuru mwenzi wako hata kama haujisikii kufanya hivyo? Si kosa, maana Kutoa shukrani ni njia mojawapo ya kupenda na hakuji kwenyewe ni lazima tutie juhudi hata wakati ambao hatujisikii kufanya hivyo. Kama utampenda mwenzi wako wa ndoa kwa kumwonyesha shukurani,basi atabadilika na kuonyesha maendeleo mazuri! Lawama na malalamiko hiviwezi kumbadili mwenzi wako, lakini shukrani inaweza. Jaribu utaona matokeo yake!
Njia ya pili
(b) Kufanya vitendo vya uungwana na ukarimu
Njia ya pili ya kupenda kwa vitendo ni kufanya vitendo vya uungwana na ukarimu, mwanzo wa ndoa yenu pengine ulikuwa mwangalifu kufanya vitendo vya uungwana na ukarimu kwa mwenzi wako, je bado unafanya hivyo mpaka sasa? Kumbuka Mungu amewaamuru waume na wake kupendana, na moja ya sehemu muhimu ya upendo ni kufanyiana vitendo vya ukarimu na uungwana, haya ni baadhi ya mapendekezo ya namna ya kutekeleza.
Ø Mweleze mkeo; “Nakupenda” halafu toa sababu maalum utaona uso wake unang’aa mara tu utajapo kitu kinachokufurahisha kuhusu yeye.
Ø Nendeni matembezini pamoja, hii itamwonyesha bado ungali unapenda kutumia muda pamoja naye; Unastarehe ukiwa pamoja na mkeo.
Ø Kila mara inapowezekana mletee zawadi mkeo, japo zawadi ndogo tu, mfahamishe kuwa zawadi hii ni kwa sababu, “nakupenda sana moyoni mwangu” nategemea unilipe kwa njia maalum usiku tuendapo kitandani”
Ø Uwe mwangalifu unapoongea naye wakati umekasirika
Ø Waeleze wazazi wake jinsi gani unavyomthamini binti yao.
Ø Tumia muda kukaa na kuongea na mkeo, mfahamishe mawazo na hisia zako.
Ø Wajulishe wanao kuwa unampenda mama yao, waache waone matendo yako ya ukarimu na uungwana, wanapotambua unavyomtendea vitendo vizuri, watamheshimu….watakuheshimu na wewe
Ø Tumia mda kuomba pamoja naye, kwa pamoja wekeni matatizo yenu mikononi mwa Mungu.
Ø Mume wako anaporudi kutoka kazini, mpokee kwa tabasamu pamoja na maneno ya furaha na uchangamfu; ambayo yataonyesha furaha uliyonayo kwa kumwona. Usimpokee nyumbani ukiwa umenuna na umeekuja uso; badala yake fanya uso wako ung’ae na wenye furaha ukifikiria umuhimu wa mumeo.
Ø Anapofanya kitendo Fulani kizuri mshukuru! Maneno mawili mazuri kuliko yote ya upendo ni “Asante sana”
Ø Waeleze wanao jinsi ambavyo unamthamini baba yao, siku moja Moringe alirudi nyumbani kutoka kazini kachoka taabani. Binti yake mdogo akasema, “Baba mama husema kwamba unafanya kazi kwa bidii sana ili kusudi tuishi vizuri hapa nyumbani.” Ghafla alisahau uchovu wake wote aliokuwa nao.
Ø Vaa nguo aipendayo na mfahamishe kwamba umeivaa nguo hiyo kwa sababu tu ni nguo anayoipenda sana.
Ø Tafuta sifa zake nzuri na uzitaje mbele yake mara kwa mara.
Ø Mara nyingine asubuhi; akiwa angali amelala, mletee kifungua kinywa kitandani; ukitumia vyombo vyako maalumu, weka sinia lako kitandani, ukiwa umevaa nguo yako maalum ya kulala ambayo inaonyesha mwili wako; na mwamshe kwa busu, kwa busu hilo tabasamu halitamtoka usoni siku nzima.
Ø Kama utasikia mtu anasema kitu chochote kizuri kuhusu mumeo mweleze, usisite ukidhani labda mumeo atajivuna.
Inawezekana haujapendelea baadhi ya mawazo haya, hili si tatizo unaweza kufuata njia yako na maoni yako uyapendayo mwenyewe kulingana na tabia, mwenendo na mila yako. Itakuwa vizuri kama kila siku utapanga kitendo maalum cha ukarimu ambacho utamfanyia mwenzi wako wa ndoa. Hii inataka juhudi na nguvu ya kutekeleza. Ukweli ni kwamba kupenda ni kazi ngumu, lakini hufanya nyumba iwe na furaha na msisimko wa mapenzi wa hali ya juu.
Njia ya tatu
(c) Mkubali mwenzi wako kama alivyo
Njia ya tatu ya kupenda kwa vitendo ni kumkubali mwenzi wako kama alivyo, hata kama anamapungufu kadhaa. Ni wazi kuwa kuna mambo mengine hatuwezi kuyakubali katika ndoa. Kwa mfano, mwenzi wako wa ndoa anazini, huwezi kunyamaza na kumwachia aendelee kufanya hivyo, badala yake chukua hatua Fulani kuzuia kitendo hicho. Au kama mwenzi wako hukupiga, hauwezi kuvumilia tabia ya aina hiyo. Pamoja na hayo sasa, katika ndoa kuna mambo mengi ambayo lazima tuyakubali, Christina alisema katika miaka mitano iliyopita amekwisha mweleza mume wake zaidi ya mara elfu moja kwamba asiache magazeti sebuleni, lakini bado anarudia, maana kila atokapo kazini huyasoma na kisha huyadondosha sakafuni, mpaka Christina ayaondoshe……...kitu cha kufanya katika hali kama hii, ni kwamba kila mtu katika mahusiano anapaswa kutambua kuwa anawajibu wa kumpenda mwenzi wake, hii ina maana kumkubali kama alivyo, uwe mcheshi na mkarimu kwake hata kama anarudia makosa ya yale uliyokwisha mweleza kuwa hayakupendezi, kwa maneno mengine ni kwamba…….Upendo huvumilia kasoro nyingi. Ukisema unampenda mwenzi wako maana yake umemkubali kama alivyo pamoja na udhaifu wake. Kisaikolojia wamaume hawapendi kuelezwa jambo la aina moja tena na tena, ukifanya hivi utaonekana kama unampigia kelele,lawama au aina Fulani ya mizozo. Kupiga kelele au lawama siku zote hazkumbadilishi mwanaume, badala yake hutamani kukimbia.
Ni afadhali kukaa katika pembe ya dari ,kuliko kukaa katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi……….(mithali 25:24)
Badala ya kuwa mgomvi au kulalamika saa zote, ni jukumu la kila mtu katika mahusiano kumpenda na kumkubali mwenzi wake kama alivyo. Kama utafanya hivyo utagundua kuwa mwenzi wako anafurahi kuwa na wewe. Mara zote ni vizuri kama utaona udhaifu au kasoro Fulani kwa mwenzi wako, usilalamike au kuwa mgomvi, badala yake mweleze mwenzi wako kwa njia ya upendo jinsi gani ungependa abadilike. Baada ya hapo, kila uonapo hatua ndogo ya maendeleo onyesha shukrani na mpongeze, hata kama hautaona maendeleo yoyote, endelea kumpenda na kumkubali mwenzi wako kama alivyo. Hii itawafanya nyote kwa pamoja kuwa wenye furaha zaidi kwenye mahusiano yenu. Jaribu kufanya hivyo utaona! Pengine unafikiri, “Yote haya ni juu ya kupenda kwa vitendo, ni mawazo mazuri kwa baadhi ya watu.” Ni rahisi kusema: Badala ya kumkosoa mwenzi wako, mwonyeshe shukurani, mpongeze na mkubali hata kama ana kasoro. Kitu kikubwa hapa ni kwamba haupaswi kuwa na wasiwasi kuhusu nini mwenzi wako atakutendea, amua kumpenda mwenzi wako hata kama inaelekea unapata upendo kidogo kutoka kwake.
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi,mwapata thawabu gani? (mathayo 5:25-25)
Usiseme kuwa haiwezekani, unaweza kumpenda mwenzi wako, siyo kwa nguvu zako ila kwa msaada wa roho mtakatifu. Anza kwa kukiri mbele za Mungu kuwa umekuwa ukishindwa kumpenda mwenzi wako kwa vitendo, kubali kuwa siyo mwenzio peke yake aliyeshindwa kupenda, bali na wewe vile vile umeshindwa. Ungama sehemu maalum uliyoshindwa. Amini kwamba mwenyezi Mungu amekusamehe kabisa kwa sababu Yesu aliteswa na kufa msalabani badala yako. Kisha mpende mwenzi wako, onyesha shukrani, fanya vitendo vya ukarimu, acha kumkosoa mwenzi wako na anza kumkubali kwa upendo.
Jambo la tano
Ndoa nyigi zimepooza na kuwa za upweke kwa sababu ya kukosa mawasiliano ipasavyo. Kuwasiliana maana yake ni kuongea kati ya wapenzi kwa uaminifu na uhuru. Endapo watu wawili wanawasiliana vizuri basi huongea pamoja juu ya matatizo yao yote, furaha, majonzi, na mawazo mbalimbali. Kama mume na mke hawawasiliani, ndoa yao huwa kama watu wawili wasiooana kuchangia nyumba moja. Tendo la ndoa huwa si kitu zaidi ya mume kuridhisha shauku yake na kutengeneza watoto, Ni lengo la Mungu, kwa mume na mke kuwasiliana, wakati biblia inaongelea juu ya ndoa ya kwanza, inasema hivi.
Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe,wala hawakuona haya, (mwanzo 2:25)
Neno uchi lina maana, a) Hawakuficha miili yao kati yao. b) Hawakuficha mawazo na mioyo yao kati yao, waliwasiliana bila kufichana chochote. Baada ya hapo dhambi iliingia duniani, tokeo la kwanza la dhambi ni mke na mume kufichana, walitumia majani kutengeneza nguo ili waweze kujificha kati yao mbele na mbele za Mungu, hadi leo hii sisi binadamu tungalitunajificha, tunafichana hisia zetu za ndani. Wakati mwanaume anahisi anaweza kupoteza kazi yake hawezi kumweleza mtu yeyoyote,hufikiria watu watamdharau kwa kuogopa kupoteza kazi. Hivyo hujifanya kutabasamu na kuongea juu ya mpira wa miguu au hali ya hewa. Kila mmoja wetu anataka kuongea kuhusu anavyojisikia moyoni mwake, tunahitaji kuonyesha tunavyojisikia hali zetu halisi kwa wengine, ndio maana wote hupenda kuwa na marafiki japo hata mmoja. Tunahitali rafiki wa kweli ambaye tunaweza kuwasiliana waziwazi bila kuogopa. Kama mke na mume hawatimiziani mahitaji yao ya kuwasiliana, tendo la ndoa la ndoa litakuwa baridi na lisilo na msisimko.
NGAZI ZA MAWASILIANO
Kuna viwango vitatu vya mawasiliano, na lengo la wanandoa linatakiwa liwe kufikia ngazi ya tatu. Ni vizuri kuanza na ngazi ya kwanza na baada ya hapo ngazi ya pili na tatu. Mke na mume wakifikia ngazi ya tatu hupata furaha isiyo kifani ya kuwa marafiki wa karibu, vile vile wakiwa wapenzi.
Ngazi ya kwanza
Mawasiliano rahisi na mepesi ni kuongelea juu ya mambo yaliyotokea siku hiyo, kwa mfano; mume unaweza kurudi toka kazini na ukamwelezea mke wako juu ya mkuu wako wa kazi ambaye alikuwa amelewa siku hiyo, na mke ukamweleza mume wako jinsi ulivyofanikiwa au ulivyoshindwa kuoka keki. Kuongelea juu ya matukio ya siku nzima ni mawasiliano mepesi na rahisi kuliko yote, kwa bahati mbaya , pamoja na kuwa rahisi, watu wengi walioona hushindwa kuwasiliana hata katika ngazi ya kwanza. Wanapokutana jioni huwa hawana lolote la kuongelea, kama wewe na mke wako mna tatizo la aina hii, ni vyema kumwomba Mungu awasaidie, na baada ya hapo anzeni kuongea! Kila siku ongea na mwenzako juu ya jambo lililokutokea siku hiyo. Hapo mwanzoni itaonekana kama ni kazi nzito sana, lakini baada ya wiki chache kupita itakuwa mazoea mazuri ambayo nyote mtayafurahia. Pamoja na kumweleza mwenzio juu ya matukio ya siku nzima ni muhimu umwonyeshe mwenzio kuwa uko tayari kumsikiliza jinsi siku yake ilivyokwenda. Unaweza kufanya hivyo kwa kumwuliza maswali, maswali ni muhimu katika mawasiliano. Kama mume anarudi nyumbani na mke haulizi “mambo yaliendaje?” basi inaelekea mke hajali, na kama mume haulizi kamwe juu ya siku yake, mke naye huhisi mumewe hampendi tena. Sote hupenda kuulizwa maswali yanayotuonyesha kuwa wenzetu wanatujali, endapo mtu ataniuliza maswali kuhusu kazi yangu au maoni yangu, huwa nafikiri hivi, “huyu ni mtu mzuri” katika ndoa vile vile tunapaswa kutumia maswali kuonyesha kuwa tunajaliana. Kuuliza na kujibu maswali juu ya matukio ya maisha yetu ya kila siku ni mwanzo mzuri wa kuwasiliana; lakini msiishie hapo, pamoja na msaada wa Mungu mnaweza kupiga hatua na kufikia hatua ifuatayo.
Ngazi ya pili
Ngazi ya pili ya mawasiliano ni kuongea juu yenu: mipango yenu ya baadaye, ndugu zenu, fedha zenu na kadhalika. Kwa mfano, mume inamlazimu kujadiliana na mkewe maswali kama haya: Shule gani tuwapeleke watoto wetu?, Je, tumwombe binamu yangu kuishi nasi?, Je, tununue gari jipya au tujenge nyumba yetu? Mnapozungumzia juuu ya masuala yanayowahusu na yanayohitaji uamzi, mnaweza kukuta kwamba hamuafikiani katika mambo Fulani, hata kama ni hivyo msiruhusu kutokuafikiana kusimamishe mawasiliano yenu, badala yake ni lazima muendelee kujadiliana juu ya swala hilo hadi mufikie mwafaka. Mwanzoni Mwa ndoa ya Goodluck na Frida walizozana juu ya mama yake na Goodluck, na walifanya kosa kuacha mjadala huo bila maafikiano, na baada ya hapo ili kuepuka mzozo zaidi, wote walianza kuwa wangalifu na kujaribu kuepuka kutaja suala la mama yake na Goodluck. Baadaye tena walizozana kuhusu fedha, kwa mara nyingine tena mzozo huo haukutatuliwa ipasavyo, hivyo walianza kuepuka suala hilo vile vile. Baada ya miaka kadhaa walijikuta wanaorodha ndefu ya masuala ambayo kamwe kamwe hawakudhubutu kuyataja kati yao, swala kama hili hupunguza kiwango kikubwa cha mawasiliano katika mahusiano, usiruhusu mizozo inadhoofisshe kiwango chenu cha mawasiliano, hivyo ni bora kutumia mawasiliano kutatua mizozo yote inayowakabili. Mnaweza kufanya hivyo kama mtanuia na kuendelea kujadiliana juu suala hilo kwa njia ya upole na ya upendo na kupinga hatua hadi kufikia mwafaka kati yenu na kupata uamzi. Mnapo tatua mizozo yenu huwa ni rahisi kuwa huru kuzungumzia swala linguine lolote linalojitokeza baina yenu. Kwa njia hiyo mtakuwa tayari kupiga hatua kufikia hatua ya juu kuliko zote katika mawasiliano.
Ngazi ya tatu
Katika ngazi hii ya mawasiliano mnachopaswa kufanya hapa nikushirikishana hisia zenu, kwa namna ambayo inakufanya ufungue mlango wa moyo wako kumruhusu mwenzi wako kuona kilichomo ndani, hivyo kukujua kiikamilifu jinsi ulivyo. Benja alimwambia mkewe, “leo kaka yangu alichukia na kunigombeza, isitoshe baba yangu naye alikuwa upande wake.” Taarifa ya tukio ni ngazi ya kwanza ya mawasiliano. Baada ya hapo Benja na mkewe wakajadiliana namna tatizo hilo la ndugu linaweza kutatuliwa, mazungumzo hayo yalikuwa ngazi ya pili ya mawasiliano, baada ya hapo mkewe akamwulinza Benja, “lakini unajisikiaje kuhusu kaka na baba yako?” Benja alijibu kuwa na wasiwasi moyoni kwa sababu ana hofu uhusiano wa familia unaweza kuharibika. Kushirikisha hisia namna hiyo ni ngazi ya tatu ya mawasiliano, ndoa huwa nzuri ajabu kama wana ndoa watafikia ngazi ya tatu ya mawasiliano. Mnapowasiliana katika kiwango hicho, furaha yenu huwa mara mbili kwa sababu furaha ya mmoja huwa ya mwenzie, na matatizo yenu hugawanywa kati na hupungua hadi nusu.
Haruni anadai kuwa yeye ni mkiristo halisi na kila mara huhudhuria kanisani pamoja na mkewe, lakini kila anapokuwa na tatizo hujiambia. “Sitaweleza mke wangu jinsi gani najisikia kuvujika moyo leo, mimi ni mwanaume hivyo mke wangu asije akafikiri siwezi kumudu shida” niwazi Haruni alisahau kifyngu kisemacho……… “Si vema mtu awe peke yake nitmfanyia msaidizi wa kufanana naye.” (Mwanzo 2:18)
Mwanaume yeyote asione aibu kuchangia hisia zake na mwenzi wake, maana kufanya hivyo hakutamsababisha azarauliwe na mkewe, badala yake ataheshimika na atajisikia huru zaidi kuchangia hisia zake na mkewe. Wanandoa wanaposhirikiana hisia zao wanakuwa wanawasiliana katika kiwango cha juu kabisa, na ndoa yao huwa ya kusisimua nay a kufurahisha ikiwaleta karibu sana kama pete na kidole.
Nijambo la kusikitisha kwamba ndoa nyingi zimeshindwa kuwasiliana katika ngazi ya tatu na baadhi yao hushindwa kufikia angalau ngazi ya kwanza, sababu kubwa hapa ni vikwazo ambavyo husimamisha mawasiliano. Na baadhi ya ndoa huruhusu vikwazo hivyo kusimamisha mawasiliano yao moja kwa moja. Vifuatavyo ni vikwazo vya mawasiliano.
a) Woga
Biblia inasema jukumu la mke ni kumheshimu mumewe, na siyo kumwogopa
“Ninyi wake , watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana” (wakoritho 3:18)
“Katika pendo hamna hofu, lakini pendo lilillo kamili huitupa nje hofu {1 Yohana 4:18}
Kwa bahati mbaya kuna waume wengine huwafanya wake zao wawaogope, woga ni adui wa mawasiliano, na mume na mke hawawezi kuwasiliana ipasavyo kama mke anamwogopa mumewe.
b) kutosikiliza
Mawasiliano hayawezi kuwepo kama hauko tayari kumsikiliza mwenzi wako anapoongea, yaani kusikiliza kwa makini! Ni vizuri wakati mwenzi wako anaongea ufikirie maneno ya kumjibu baada ya yeye kumaliza kuongea. Ilikumfanya mwenzi wako ahisi unampeenda kwa kutilia maanani anachoongelea na kumsikiliza kwa makini, na baada ya hapo kama hauna uhakika anachomaanisha, ni wajibu wako kuuliza; Je, una maana kusema….?, hakika kusikiliza kwa makini ni kazi, lakini unalazimika kufanya kazi na ukishindwa kusikiliza kwa makini, basi utamvuja moyo mwenzi wako.
c) Kazi nyingi
pamoja na kuwa na kazi nyingi, ni muhimu mume na mke kutenga mda kwa ajili ya mazungumzo baina yao.
d) Wajibu wa baba na mama
Mwanzoni mwa ndoa ya Yassin na Glory kwa hakika walifurahia kuwasiliana baina yao, kila mmoja wao alijisikia ni furaha ilioje kuwa na mwenzi wa ndoa ambaye unaweza kuongea naye juu ya jambo lolote lile. Lakini baada ya kupata watoto, Glory alikuwa akishughulika na malezi ya watoto, Yassin naye alikuwa kazini ili achume fedha kwa ajili ya kutunza familia. Watoto walichukuwa mda wao mwingi kiasi kwamba walianza kuzorotesha mawasiliano kati yao, hivyo uhusiano wao ulianza kupooza na kuwa baridi usiokuwa na msisimko. Ndoa za aina hii ni nyingi hata katika nyumba ambazo mume na mke ni wakristo, lakini kwa hakika huo sio mpango wa Mungu, kwamba mume azingatie tu harakati za kutafuta fedha kiasi cha kukosa mda wa kuwasiliana na mkewe, vivyo hivyo na mke naye hapaswi kuegemea kwa watoto na kukosa mda wa kuwasiliana na mumewe.
c) kuumia moyo
Moja ya vipingamizi vikubwa vya mawasiliano ni kuumia moyo, Wenzi wa ndoa wanaweza kuumizana moyo kwa urahisi, hata uchungu kidogo unaweza kusimamisha mawasiliano katika ndoa yako. Asubuhi moja wakati Kamuli anaelekea kazini, aliendelea kuwaza juu ya jambo ambalo Marco alikuwa amelisema asubuhi hiyo, ambalo lilimuumiza, hata hivyo halikumuumiza sana bali kidogo tu. Ukweli ni kwamba sio maneno ya Marco yaliyomuumiza bali jinsi ambavyo Marco alivyokaza sauti yake wakati anaongea. Pamoja na hayo, alivyoendelea kufikiria juu ya kuumizwa huko, uchungu moyoni mwake uliendelea kukua, na alikumbuka nyakati nyingine pia ambazo mumewe alikuwa amemuumiza. Alipokuwa njiani kurudi nyumbani toka kazini Kamuli aliendelea kujiuliza nifanye nini kuhusu kuumizwa huku? Naweza kusahau jambo hili. Hapana, kama nitafanya hivyo, mawasiliano yangu mimi na Marco jioni hii yatakuwa hafifu; na bado nitaendelea kuumia moyoni. Labda ni msubiri atamke, `samahani`. Hapana, hiyo, haiwezi kusaidia kwa sababu inawezekana asiwe ametambua kuwa ameniumiza rohoni., kuna jibu moja tu hapa. Lazima niongee naye kuhusu alivyoniumiza moyoni, lazima nimweleze jinsi ninavyojisikia, lakini nitazungumza naye kwa upole na kwa uwazi.” Jioni baada ya watoto kulala, Kamuli na mumewe walikuwa wamejipumzisha sebuleni, kwa aibu, Kamuli alianza kuongea. “Mpenzi nafikiri inafaa nikujulishe kuwa niliumia moyoni leo asubuhi kwa jinsi ulivyoongea na mimi, haikunipendeza. Ukweli ni kuwa nimejisikia kuumia moyo siku nzima. Lakini nimetambua kuwa haukukusudia kuniumiza, na sasa naona aibu swala dogo kama hili kunibughudhi kutwa nzima.” Na baada ya mazungumzo hayo Kamuli na mumewe walijisikia marafiki zaidi, na penzi lao jioni hiyo lilikuwa zuri mno.
Ni vizuri wana ndoa kuwa waangalifu kuchangua mda sahihi na mahali panapofaa kumweleza mwenzi wako juu ya jambo linalokutatiza, na sio wakati wowote. Mda unaoofaa ni ule ambao mnakuwa mmepumzika, na siyo wakati ambapo mwenzi wako anakuwa amechoka au ana njaa. Mahali panapofaa ni pale mnapokuwa mmekaa wawili kwa faragha pasipo kusumbuliwa na kelele yoyote. Vilevile mtahitaji mda wa kutosha kumaliza maongezi bila kukatizwa. Ni muhimu mume na mke kutilia juhudi katika kujenga mawasiliano kati yenu.
Baada ya miaka 5 katika ndoa na mume wangu na watoto 2, mume wangu alianza kufanya tesa na kutoka nje na wanawake wengine na akanionyesha mapenzi baridi, kwa mara kadhaa anatishia kunitukana ikiwa nitathubutu kumuuliza juu ya uhusiano wake na wanawake wengine, mimi iliharibiwa kabisa na kuchanganyikiwa hadi rafiki yangu wa zamani akaniambia juu ya simulizi ya spell kwenye wavuti inayoitwa Dr.Wealthy ambao husaidia watu walio na uhusiano na shida ya ndoa na nguvu za miiko ya upendo, mwanzoni nilitilia shaka ikiwa jambo kama hilo litakuwapo lakini aliamua kujaribu, nilipowasiliana naye, alinisaidia kutoa upendo na ndani ya masaa 48 mume wangu alirudi kwangu na kuanza kuomba msamaha, sasa ameacha kwenda nje na wanawake wengine na wake pamoja nami kwa uzuri na kwa kweli . Wasiliana na cell hii kubwa ya upendo kwa uhusiano wako au shida ya ndoa kutatuliwa leo kupitia: wealthylovespell@gmail.com au moja kwa moja WhatsApp: +2348105150446.
ReplyDeleteMaisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma
ReplyDeleteKwaheri Gerd Ulrich
Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe nikiwa nimesimama peke yangu bila mwili kusimama na mimi na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na mchawi huyu wa hodari Dk. ASUBUHI, baada ya kumueleza hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi akiniomba kuwa hatawahi. niache tena, miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa pia una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
ReplyDelete*penda uchawi
* kama unataka ex wako nyuma
* Acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa ulinzi
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
Wasiliana na Dk DAWN kwa barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159
Habari zenu. Ilikuwa ngumu sana kwangu wakati mpenzi wangu aliniacha kwa mwanamke mwingine. Niliharibiwa kihisia, nilivunjika moyo na sikujua la kufanya ili kumrudisha. Nilihangaika kwa miezi mingi na niliendelea kutafuta msaada kutoka kila mahali hadi nilipopata kujua kuhusu DR DAWN. Niliwasiliana naye na kumweleza shida zangu. Alikuwa tayari kunisaidia na kunisisitiza nifuate taratibu ili aweze kurejesha penzi kati yangu na mtu wangu na pia kuhakikisha tunarudiana wote wawili. Nilipata mahitaji yote na ilifanya kazi hiyo. Baada ya saa 48, nilipata ujumbe kutoka kwa mpenzi wangu akiniuliza tarehe. Sasa tuko pamoja tena na shukrani zote kwa DR DAWN. Anaweza kukusaidia kumrudisha mpenzi wako,
ReplyDeleteAnaweza kukusaidia na uchawi wa ujauzito,
Anaweza kukusaidia kuponya aina yoyote ya ugonjwa.
ikiwa uko tayari kuamini na kubaki na matumaini. Watumie barua pepe tu kupitia: dawnacuna314@gmail.com
WhatsApp: +2349046229159
Nilikuwa na uzoefu mgumu na wa kutisha katika mahusiano yangu ya awali na nilisubiri sana hadi nilipokutana na mume wangu na baada ya kukutana, tulipendana na kuoana. Baada ya miaka miwili ya muungano, alibadilika na kuanza tabia za ajabu na hatimaye kuniacha mimi na mtoto wetu. Nilifanya kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilipata maoni mengi na kila mtu alikuwa akisema juu ya Dk Dawn. Niliwasiliana naye na alinijibu na kunipa juhudi zake zote na msaada ili kuifanya ndoa yangu ifanye kazi tena. Yeye ndiye aliyenijulisha kuwa mume wangu alichukuliwa kutoka kwangu na mwanamke mwingine na akafanya uchawi wa kuungana tena ambao uliturudisha pamoja na kurudi nyumbani kwangu na kijana wangu. Hakika, hakuna mtu huko alidanganya kuhusu Dk Dawn na matendo yake mema. Mume wangu alirudi nyumbani saa 73 baada ya kufanya kazi kama alivyoahidi. Wasiliana naye sasa na uwe na uhakika kwamba atakusaidia kuunganisha tena ndoa/uhusiano wako.
ReplyDeleteAtakusaidia kushinda kesi mahakamani au kulipiza kisasi dhidi ya adui zako.
Atakusaidia kuponya ugumba na kila aina ya magonjwa/magonjwa.
Ana suluhisho la shida yako.
Wasiliana na Whatsapp yake: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com